Pages

Monday, July 29, 2013

UNAYAJUA HAYA YENYE UMUHIMU KUHUSU FEDHA KATIKA NDOA ??


   
    Tafiti nyingi zinaonesha kwamba migogoro mingi ya wanandoa hutokana na mambo yanayohusu pesa.
Pia mfumo wetu dume katika jamii umeongeza tatizo kuwa kubwa zaidi kwani suala la pesa ameachiwa mume bila mke kuwajibika, kujua au kuchangia lolote, hata wanawake wenyewe wengi wamejiweka katika kundi la kuwaachia wanaume kuwajibika kwa kila kitu kinachohusu pesa katika na kutoa maamuzi yote yanayohusu pesa katika ndoa.
Na kuna maamuzi mengine yameangamiza familia kwa sababu ni mtu mmoja tu katika ndoa ndo hutoa maamuzi linapokuja suala la pesa yaani baba au mume.

Sasa ulimwengu umebadilika wanawake nao wana uwezo, wanafanya kazi, wanaingiza pato katika familia na ndoa.
Pia kuna familia ambazo mke ndiye mwenye kipato kikubwa kuliko mume, na kuna ndoa ambazo kila mmoja akipata pesa hutumia anavyotaka yeye bila kukaa pamoja na kupanga nini kifanyike na matokeo yake kumekuwa na migogoro ya hapa na pale na kusuguana kwa hapa na pale.
mambo yafuatayo ni muhimu sana kuwekwa wazi kwa wanandoa kwa ajili ya kuimarisha ndoa hasa linapokuja suala la fedha.

Kuwa na Account Moja:Kitu kikubwa ambacho wana ndoa wapya hukupamba nacho mara wakishaanza maisha pamoja ni jinsi ya kupangilia matumizi ya pesa.
Kama wote mnafanya kazi, je ni muhimu kuwa na account moja ya pesa? au kila mmoja kuwa na account yake then wote kuwa na account ya tatu ya pamoja?

Asilimia kubwa ya wanandoa wapya hufungua Account ya pamoja wakishaoana .

Kitu cha msingi ni kuhakikisha mmekuwa kitu kimoja si katika mwili mmoja tu, bali hata katika pesa.
Kuwa na account moja ni sawa, pia kuwa na account tofauti ni sawa.
Kitu cha msingi ni kuwaelewana juu mapato na matumizi ya pesa zenu na pia malengo ya kiuchumi ya muda mrefu na muda mfupi, kama kuwekeza na akiba kwa pamoja.
Pia kujua aina ya matumizi ya pesa kwa kila mmoja kwani kama mmoja ni mtumiaji na mwingine ni mtu wa kuweka akiba, mnahitaji kujuana ili kusiwe na kinyongo kwa mmoja.

Pia kama mmoja wenu ameingia kwenye ndoa huku anadaiwa na Bank ni vizuri kumjuulisha mwenzake kwani kuoana ni pamoja na hilo deni mnakuwa kitu kimoja.
Kuna wengine wanaingia kwenye ndoa huku tayari walishawekeza kwa ajili ya mke/mume na watoto aliokuwa anatarajia.
Kitu muhimu ni kuwa wazi kuhakikisha mke wako au mume wako anajua.

Jinsi ya Kupambana na MadeniKatika mambo yote ya pesa katika ndoa, madeni ni jambo linaloongoza kuleta zogo mwenye ndoa na kama hamjafahamishana vizuri inaweza kuleta maafa.
Pia mara nyingi wana ndoa huwa wanatofautiana katika mtazamo kujua lipi ni deni kubwa au dogo hasa kutokana na elimu ya fedha ya kila mmoja.

Hilo ni deni lenu wote hivyo lazima muweke mikakati ya kuondokana nalo kwa pamoja.
Mara nyingi wengi hujiingiza katika deni bila upande mwingine kujua hali ikiwa mbaya ndiyo mtu anaanza kutoa taarifa kwamba ilikuwa hivi na vile huku nyumba inataka kuuzwa au kufukuzwa kazi.
Hapo ndiyo zogo huanza na ndoa huanza kuyumba kwani upande mwingine hujiona hauthaminiwi.

Mmoja kuwa Mtumiaji wa Pesa zaidi ya Mwenzake.Wanandoa wengi hulaumiana kwamba "wewe ni mtumiaji mbaya kuliko mimi" au kumtuhumu mwenzake kwamba anatumia pesa katika kununua vitu visivyo muhimu katika maisha.

Jinsi ya kutumia pesa huleta maneno katika ndoa nyingi, wapo wanaume akipata pesa tu ni kwenda kununua TV kubwa, Music System na vitu vingi vya starehe wakati mke anataka Pesa ya kununua kiwanja amechoka kukaa nyumba ya kupanga, au mwanamke yeye ni kununua nguo za fasheni mpya iliyoingia mjini hata kama ni gharama kubwa wakati mtoto anahitaji ada ya shule.
Kitu cha msingi ni kuwa na malengo ya muda mrefu na muda mfupi na kwamba kuwa na uelewano wa kujua nini kinunuliwe (bajeti).
Kuvaa ni muhimu na pia kuwa na vitu vya starehe ndani ya nyumba ni muhimu ila kupanga malengo na kuwa na mawasiliano mazuri hilo ndiyo jambo la kwanza.
Kaa pamoja, panga vitu vya msingi,
Tununue nini na kwa nini?
Tuwekeze wapi? na kwa nini?
Tuweke akiba kiasi gani kila mwezi na kwa nini?

Panga pamoja kila mmoja aelewe kwa nini hiki kinafanywa Badala ya hiki.

Kuwekeza kwa Busara na Hekima:
Mustakhabali wa maisha yenu ya miaka 5, 10, 20. 30, 50 ijayo ni sasa na jinsi mnavyotimia pesa na kupanga malengo.
Kuwekeza pesa katika business mara nyingi huwa na risk na risk ikitokea mara nyingi mmoja huanza kumlaumu mwenzake kwamba wewe ndo ulilazimisha tufanye hivyo.

Ni muhimu kushirikiana katika kuweka uamuzi wa pamoja mnapowekeza pesa kwenye miradi au business pamoja.
na piakukubaliana risk yoyote ikitokea pamoja kwani kama ni faida ni yenu wote na kama hasara ni yenu wote.
Katika hali ya kawaida katika ndoa inaonesha kwamba wanaume ndo wanaongoza kwa kujitosa kufanya kitu chochote (business) hata kama kuna risk kubwa baadae na wanawake huogopa sana kuwekeza katika kitu ambacho hawana uhakika.

Kitu cha msingi ukitaka kufanikiwa katika business au maisha lazima uwe risk taker kwani ukifanikiwa unaweza kubadilisha uwezo wa kifehda wa familia yako, ingawa unahitaji kufanya utafiti mkubwa kabla ya kuwekeza pesa zako na uwe na njia ya kupunguza risk inapotokea au Usibebe mayai yote kwenye kikapu kimoja kwani kikidondoka umeumia.
Kutunza Siri zinazohusu pesa
Wengine wanaamini siri za pesa walizonazo bila mume au mke kujuahazina ubaya sana kwenye ndoa.
Ukweli ni kwamba unahatarisha sana ndoa yako kwa kuficha siri za pesa ulizonazo au business unazofanya bila mke au mume kujua.
Wengine wameficha wake au waume fedha walizonazo katika Account walizonazo
Wengine hata wakinunua vitu hudanganya bei waliyonunulia vitu.
Na wengine hujiingiza katika business ambazo mke au mume hajui na huko ikitokea hasara au tatizo ndo hurudi kusema kwa mke au mume, hapo ndo zogo linaanza.

Wengine huwapa ndugu zao au marafiki zao pesa nyingi bila mke au mume kujua na siku mke au mume akijua kwamba mmoja alitoa pesa bila kuambiwa hapo tena moto unalipuka.
Ni muhimu kutoficha siri zozote kwa mke au mume wako kwani lolote linaweza kutokea wakati mwingine hata kifo, utatesa watoto bure kwa kuficha siri muhimu kama hizo ambazo si siri bali jambo muhimu kwa mke au mume wako.

Kupanga kwa ajili ya fedha ya dharuraWengi hudhani haina haja kuwa na pesa ya dharura
Na wengine hupanga fedha ya dharura kwani chochote kinaweza kutokea, anaweza mtoto kuugua au ninyi wenyewe mmoja kuugua ghafla pia kunaweza kutokea mchango wa dharura bila kujua.
Hata kama una kazi nzuri kama hujajipanga vizuri kwa ajili ya mambo ya dharura unaweza kushangaza mke au mume kwani lolote laweza kutokea.

Matatizo hayataisha hadi tuwe tumekufa, kupangilia vizuri masuala ya pesa kutawezesha ndoa yako kuwa yenye afya na imara.







Kwa hisani ya Mbilinyi.



No comments:

Post a Comment