Kuna baadhi ya wanaume hawajui jinsi ya kuzungumza na mwanamke au msichana. Kwa njia hii wanaume wengi wanaishi maisha ya bila kumvutia mwanamke yeyote.
Hapa kunanjia 15 utakazozitumia wewe mwanaume ili kuhakikisha humkwazi mwanamke unayempenda mnapokuwa katika mazungumzo ;
1. Wakati
ukizungumza nae, jaribu kuzungumzia "hisia" kama vile kumbu kumbu yako
ya utotoni, matarajio ya baadae au matamanio yake. Mada hii ya
mazungumzo yenu yatafungua milango ya hisia zake ghafla.
2. Wanawake
huhitaji mwanaume asiyekuwa na uoga wa kuwamiriki na kuwaongoza. Wakati
unazungumza na mwanamke tawala mazungumzo yenu na kamwe usimpe nafasi
ya yeye kuanza kufikiri kuwa nini ulichokuwa ukizungumzia.
3. Kuwa
makini wakati unapokuwa ukizungumza nae huku akikupatia majibu yasiyo
na hisia zozote za mapenzi. Hapo utajua kunakitu, hivyo kama kwa bahati
mbaya uko nae karibu kiasi cha kugusana, basi jisogeze pembeni wakati
ukiwa unaendelea kuongea ili asishtukie au unaweza kumuona hayuko sawa
katika utoaji majibu.. kwa kawaida atakuonyesha ishara, hivyo kuwa nazo
makini.
4. Kumbuka hii kauli mbiu "Ucheshi/vituko ni mapenzi". Wanawake huvutiwa sana na wanaume wanaoweza kuwafanya wawe na furaha muda wote. Usijikite zaidi katika kufanya utani unaopita kiasi na kusahau ulichokuwa unaongea. Bali jikite zaidi katika mambo yanayomfanya ajisikie kuwa na msisimko na starehe wakati ukonae.
5. Zama
katika undani wa mazungumzo baina yako na yeye. Mwanamke huendana na
mwanaume asiyekuwa muoga wa kuzungumzia mambo binafsi kwa ukaribu.
6. Wanawake
wengi hupenda kujua maoni yako kuhusiana na jinsi unavyomuona. Mwambie
vitu unavyoviona kutoka kwake, lakini jaribu kuwa makini ili usitamke
vitu vingine vitakavyo msababishia apoteze furaha.7. Epuka
kumpa ofa nyingi mwanamke, mwanamke huwa na mashaka na mwanaume
anayempatia vitu vingi kwa wakati mmoja ama kila mara. Kwasababu
atafikiri vitu unavyompatia ni kutaka kumvutia tu ili umpate kiurahisi.
Kitu ambacho baadae kitaleta madhara makubwa.
8. Kama
unahitaji kujua njia nzuri ya kuweza kuongea na mwanamke au msichana
bila kumfanya asikudharau au kuboreka, basi usitumie njia ya kumuuliza
maswali mengi katika mazungumzo yenu. Bali jaribu kueleza mawazo yako
kuhusu vitu flani.
9. Kumbuka
kauli juu ya kuuliza maswali: Badala ya kumuuliza "wewe umekulia
wapi?", uliza "unaonekana kama hujakulia maeneo haya!" Hii itakusaidia
wewe kufanya uchunguzi juu yake bila yeye kujua.
10. Usifiche
utambulisho wako - zungumza vitu kutoka katika hisia zako, onyesha
uhalisia wako katika kuzungumza na usitumie mikogo ya mtu yeyote.
Njia bora ya kufikiria jinsi ya kuzungumza na mwanamke, ni kutambua
njia sahihi ya mazungumzo ya furaha na yakimahaba utakayopenda kuitumia,
isipokuwa usimuige mtu. Kuzungumza na mwanamke sii vigumu bali nikujua
ni vitu gani hasa mwanamke hapendi kuvizungumzia na vitu gani anapenda
kuvisikia. Fuata maelekezo hapo juu utaona matunda yake...kisha rudi toa
maoni yako hapa.
MUHIMU: Maelekezo
haya yote yatafanikiwa kwa mwanamke mwenye kuhitaji mapenzi ya kweli -
yani sio kwa wanawake wanaolenga kuchota pesa kwako na kutokomea. Hivyo
kuwa makini sana.
No comments:
Post a Comment