Pages

Saturday, June 21, 2014

JE UNAZIJUA NGUZO MUHIMU ZA NDOA YEYOTE ILE ??




1. SIRI - Ukiwa katika ndoa, siri ni kitu muhimu sana ambacho huenda ukikifuata kitakuepusha na mambo mbali mbali yatakayosababisha ndoa yako iteteleke. Chagua watu maalumu unaowaamini ili uwatumie katika kuomba ushauri kwamfano, wataalamu wa mambo ya ndoa au saikolojia, ndugu wa karibu au rafiki yako wa karibu sana, na wale wote unaowaamini. Ukifanya hivyo utawaepuka wale wote wenye nia mbaya na ndoa yenu.




2. KUWA MUWAZI KWA MWENZIO -
 Binadamu tumeumbwa tofauti tofauti, huenda kitabia pia tukawa hatujakamilika kuweza kumudu hali tofauti tofauti zinazotukabili katika maisha yetu, lakini yote hayomwisho wa matatizo ni kuwa muwazi, kwani wahenga walisema; mficha maradhi kifo humuumbua. Mwelezemwenzi wako pale alipokosea ili ajirekebishe, kuliko kukaa kimia rohoni bila kusema.



3.JIFUNZE KUOMBA MSAMAHA UNAPOKOSA - 
Hakuna suluhu nzuri na nzito kama kuomba msamaha pale unapokuwa umekosa, maana ukithubutu kufanya hivyo kwa mwanadamu mwenzio, hata kwa Mungu utasamehewa. Jishushe pale mwenzio anapokuwa na ghadhabu juu yako, pengine unaweza kuwa hujakosa, lakini kushuka kwako kunaweza kukamfanya mwenzio ajutie kosa endapo kweli kama atakuwa amekosa. Lakini pia endapo ukijua wewe ndiye mwenye makosa, basi omba msamaha ili kuokoa muda.


4. MCHUKULIE MWENZI WAKO KAMA PACHA WAKO - 
 Mara nyingi umri wa wanandoa hutofautiana sana au kidogo, lakini unapokuwa tayari katika ndoa, vipengele hivi hupotea. Ni vizuri ukamheshimu mkeo au mumeo kwasababu ya ndoa yenu na sio kigezo tu cha umri. Kuna baadhi ya wanaume kuwachukulia wake zao kama watoto na kutoa amri mbaya hata mbele ya watoto wao, hupaswi kufanya hivyo, kwani huo utakuwa ni unyanyasaji wa kijinsia.  



5. KUWA MSAFI  -
 Unapoamua kuwa msafi, sio kuishia katika nguo na mwili wako tu, bali hata kwa watoto wenu pia. Hakikisha nguo za familia zinakuwa safi, na sio kurundika nguo chafu ndani kwa wiki nzima au kuloweka nguo wiki nzima. Uzuri wa nyumba ni pamoja na usafi.






6. MTUMAINI MUUMBA WAKO NA MEMA UTAYALA - Ndoa yoyote ile inayomcha Mwenyezi Mungu, itadumu hadi mwisho wa maisha yao. Wanandoa mnapaswa kumuhofu Mungu wakati wote, kwani mkifanya hivyo mtazibwa macho ya usariti, kiburi, michepuko na hata matamanio yaletayo magonjwa katika ndoa au familia yenu.





... "MICHEPUKO SIO DILI".....Baki Njia KUU !!

No comments:

Post a Comment