CAMPAIGN AGAINST FISTULA IN TANZANIA

 
Obstetric Fistula ama shimo la uzazi ni tatizo la kiafya ambalo ni kubwa sana haswa katika nchi zinazoendelea; Tanzania ikiwa moja wapo, sehemu za vijijini zaidi - ikiwa na wanawake wengi haswa wadogo wenye hili tatizo la shimo la uzazi.
Shimo hili la uzazi hutokea pale muda wa mama wa kujifungua unapokuwa umekaribia, hivyo mwanamke anakuwa ana sikia labor pains halafu mtoto anataka kutoka lakini anakuwa amebanwa kichwa. Tatizo hili linapotokea husababisha mishipa ya sehemu za uzazi kulegea na kushindwa kufanya kazi muhimu kama ya kubanisha mkojo na choo kikubwa. Hivyo mwanamke mwenye hili tatizo hujikuta anatokwa na mkojo na choo wakati wowote.
Kuna shimo la mbele la uzazi na shimo la nyuma. Shimo la mbele huitwa - Vesico-Vaginal Fistula (VVF) -shimo hili hutokea katikati ya vagina (uke) na bladder (mfuko wa mkojo).
Na shimo la nyuma ambalo huitwa - Recto-Vaginal Fistula (RVF) hutokea katikati ya vagina (uke) na utumbo unaohifadhi choo kikubwa.
 

 

Tuchangie katika kuwasaidia wanawake kupata matibabu ya haraka ya fistula hapa Tanzania kwa kutoa elimu juu ya ugonjwa huu na kuchangia kifedha harambee za kuwalipia wanawake wanaohitaji matibabu katika hospitali zetu....MUDA NDIO HUU......TATIZO ILI NI LETU SOTE.



Mwanamke anayesumbulia na tatizo la fistula akiwa hospitalini akisubiri matibabu.

0 comments:

Copyright © 2013 Owned and Managed by Bouner Disneysorata Tanzanite! All right Reserved..