JE KUNATOFAUTI KATI YA NDOA NA HARUSI ?




Ndoa ni muungano kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mume na mke muda wote wa maisha yao. (Sheria ya ndoa – mwaka 1971 kifungu cha 9).

i) Wanaooana wawe wamekubaliana pasipo kulazimishwa na mtu.ii) Ndoa ni ya mwanamke na mwanamume.iii) Ni ndoa ya kudumu maishani.

Je Harusi ni nini?

Anaandika Amicus Curiae

'' Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi!

Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza ndoa picha inayowajia ni Suti kali, Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, Mashosti kuingia ukumbini na Wimbo wa Alingo,Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokua kali pale Karimjee Hall.. 
Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?? Umewahi kuwaza Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?? Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi. 
Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika. Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo... Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kwa mumeo??? Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?? Sidhani... Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,Unatamani Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi????  ''

                                       JE WEWE UNAONAJE? UPO UTOFAUTI AU LA ?


0 comments:

Copyright © 2013 Owned and Managed by Bouner Disneysorata Tanzanite! All right Reserved..