Habari Wadau wetu wa Twende Harusini Blog !
Mada kuu leo.
mara nyingi wasichana huwa tunavikwa pete siku ya engagement day!! sasa endapo hitatakiwa mvulana/mchumba umzawadie msichana kitu tofauti na pete, Je utampa msichana/mchumba huyo nini ?? na hendapo msichana naye atatakiwa ampe mvulana zawadi baada ya kuvishwa pete atatakiwa ampe zawadi gani mchumba wake huyo?!
KARIBUNI SANA TUCHANGIE MAONI.
HAPO CHINI NI AINA MBALIMBALI ZA PETE ZA UCHUMBA.
Sometime you may try this kubadilisha mazoea ya ulazima wa keki kutengenezwa na ngano,mayai,sukari nk.
The meaning of RSVP in English is Please Respond. It literally is a French abbreviation for Répondez Vous Sil Vous Plaît or "respond you please". On a wedding invitation, the meaning of writing RSVP is that the couple is asking you to reply promptly, typically using an enclosed response card. Sometimes they'll ask you to respond by telephone or email. You can also reply on your own stationery, which is the most formal and traditional method
Does RSVP Mean You Have to Respond If You Can't Attend?
RSVP means respond either way. An engaged couple need to know as soon as possible if you can or can't be there. They've probably had to make hard choices about their guest list, and they may be waiting to see how many of their original invitees decline before sending out a few additional invitations.
Why You Need to RSVP On Time?
You'll often see, "RSVP By [a certain date]" or, "The favor of a reply is requested by [a certain date]." Your hosts have selected the date that allows them to have enough time to plan and prepare. They need to know in advance how many seats, tables, programs, and favors they'll need. Most importantly, caterers require exact numbers, and charge extra for last minute changes. Ideally, you'll have responded as soon as possible, long before that date.What If You Don't Know If You Can Be There?
Sometimes the RSVP date comes and you still don't know if you'll be able to be there. You may still be trying to find affordable travel arrangements, a babysitter, or time off from work. When I'm in this situation, 9 times out of 10 I decline. My reasoning is that if I truly wanted to be there, I would have figured out a way long before the deadline. If they're close friends, I'll phone the hosts with profuse apologies, explain the situation, and ask if the reply date has any flexibility. That way they're not forced to track me down, or wonder if I'm coming. However, this approach should be used with discretion. If every guest asked for flexibility, the hosts would be completely overwhelmed.
The Bottom Line
RSVP means please respond, and that's exactly what you should do. Tell them that you've received their invitation, and let them know if you'll be there as soon as possible. Nobody likes to be kept waiting, especially for something as important as their wedding.
Baada ya kuvishwana pete ya uchumba,
wasichana wengi huona kwamba kilichoko mbele yao ni kupanga harusi tu.
Hujishughulisha kwa hali na mali kuhakikisha harusi inakuwa sawa na ile
anayoiwaza siku zote, na kusahau kuwa baada ya harusi kuna maisha ambayo
ndiyo haswa yanayopaswa kupangiliwa kwa umakini. Baadaye wanajikuta
wameingia kwenye ndoa huku mambo mengi yakiwa hewani na hivyo kupelekea
migogoro isiyoyalazima mara tu baada ya ndoa.
Kuna mambo muhimu sana ambayo wachumba
wanapaswa wayaongelee na kufikia muafaka kabla ya kuunganika na kuwa
mwili mmoja. Yanaonekana ya kawaida sana lakini yanaweza kuleta msuguano
na kuharibu kabisa furaha ya ndoa. Tuyaangalie kwa uchache:
1. Mahali pa kuabudu.
Binti anaabudu katika kanisa kubwa na ndiye kiongozi wa sifa na muongozaji wa nyimbo karibia zote za kwaya, na kijana anaabudu kwenye kanisa dogo linaloanza na ndiye mwenyekiti wa vijana na mwalimu wa shule ya jumapili. Hapa nani anamfuata nani? Bila kukaa chini na kujadiliana kwa pamoja jambo hili linaweza kuleta mvutano. Ni vyema mkaangalia kwa mapana na marefu option zote kisha kwa pamoja mfikia muafaka kulingana na huduma ya kila mmoja wenu.

2. Jinsi ya Kuishi
Waafrika ni kawaida yetu kuishi pamoja na ndugu zetu na kusaidiana katika mambo mbalimbali ya maisha. Sio jambo geni kumkuta kijana au msichana anaishi na wadogo zake na kuwasomesha. Linapokuja suala la ndoa ni vyema jambo hili likawekwa sawa mapema. Je mtaweza kuishi na ndugu wangapi? Na wa upande upi na kwa kigezo gani? Je wataanza kuishi nanyi muda gani baada ya kuoana? Pale tu mtakapooana au lini? Hili si jambo dogo na linaweza kuharibu amani kabisa ndani ya nyumba. Ni vyema mkaliweka sawa mapema na wale mnaoishi nao wajue hawaishi tena na kaka au dada bali Mr & Mrs hivyo heshima iwe kwa wote. Pia sishauri kuishi nao mara tu baadavya kuoana, ni bora wakaenda kwa ndugu wengine angalau mwezi mmoja wa kwanza muweze kuwa na wakati wenu wa faragha wa kufahamiana vizuri na kuizoea nyumba yenu mkiwa wenyewe.

3. Mapato na Matumizi
Hili ni eneo nyeti sana. Wasichana wengine wanapoolewa huambiwa kuwa ‘usimwambie mumeo unapata kiasi gani na uwe na akaunti yako ya siri.’ Mmh hapa pana tatizo, maana nijuavyo mimi mwili mmoja ni katika kila idara, hamna siri. Sasa wewe ukificha na mwenzio akaficha, kuna maendeleo kweli hapo? Ni muhimu sana kwa wachumba kukaa na kupanga jinsi ya kuyatumia mapato yenu mtakapooana. Muwe wawazi kila mmoja anachokipata na muainishe matumizi yenu na kuangalia ni kwa jinsi gani mtaweza kuyafanikisha.

Baada ya kuoana, kila kitu kitakuwa ni
chenu wote. Kama ulikuwa na nyumba, gari, viwanja, shares, bank accounts
n.k vyote vinakuwa mali ya familia, hivyo ni vyema mkaangalia hili
mapema ili asije mmoja wenu akajenga nyumba kwa siri bila mwenzie kujua.
Pia muangalie ni ndugu gani wanahitaji msaada kifedha na jinsi gani
mtaendelea kuwasaidia, mfano ada, matibabu, n.k. Hapa panahitaji hekima
kubwa sanabya kiMungu kuamua nani asaidiwe kulingana na kipato chenu kwa
wakati huo. Maana ndugu wa kuhitaji msaada wenu watakuwa ni wengi
kuliko uwezo wenu.
4. Mipango ya Mbeleni
Shule, ujenzi, kuanzisha familia, kufungua biashara, kuanzisha huduma n.k yote haya yanahitaji kuzungumziwa mapema na kuwekewa misingi. Mfano wewe unahitaji baada tu ya ndoa utafute scholarship ukasome ulaya wakati mwenzio akifunga macho tu anajiona anaitwa baba, hapo lazima shida itatokea. Lazima mjue vipaumbele vyenu kama familia ni nini. Mkishafahamu hilo ni rahisi kujua muanzie wapi na wakati gani. Mume hawezi tu kuamka asubuhi na kusema anaacha kazi na kuanzisha kanisa, sasa familia itakula wapi? Ni lazima mkae chini mpange mjue mume akiacha kazi familia itaishije, mke je atakuwa tayari kubeba majukumu yote?

Mwisho huu ndio wakati muafaka kumweleza
mwenzio kama uliwahi kuchumbiwa hadi kutolewa mahari lakini mambo
yakaharibika. Pia kama unamtoto ni lazima narudia LAZIMA umweleze mwenzi
wako. Usiingie kwenye ndoa na siri yoyote, itakuwa ni bomu la
kuwasambaratisha.
Kwa hisani ya Magreth Riwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)