EMELDA MWAMANGA AWAHAMASISHA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KUJIAMINI.
Akizungumza wakati wa semina ya wanawake wajasiriamali iliyoambatana na maonyesho ya bidhaa mbalimbali jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Afisa mtendaji mkuu wa taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Dare to Dream foundation iliyoandaa semina hiyo Emelda Mwamanga alisema kutojiamini ni moja kati ya sababu zinazowafanya wanawake wajasiriamali kushindwa kusonga mbele
Emelda alisema kuwa, duniani ya sasa ya kibiashara imejaa ushindani
mkubwa na bila kujiamini itakuwa ni vigumu kwa wanawake wajasiriamali
kuweza kufanikiwa.
"Semina hii imewaleta pamoja wanawake wa kada mbalimbali ili kuweza
kubadilishana uzoefu pamoja na kutiana moyo. Wapo waliofanikiwa
kibiashara ambao watawaeleza wale ambao bado hawajafanikia njia
walizopitia mpaka kufika hapo walipo. Kupitia semina hii watajifunza na
namna ya kutengeneza bidhaa zenye viwango pamoja na namna ya kujitanga,"
alisema
Kwa upande wake Afisa masoko wa benki ya CRDB Emmanuel Kiondo alisema
kuwa benki yake inatambua umuhimu wa kumwezesha mwanamke na ndiyo maana
ikaamua kujitokeza kudhamini shughuli hiyo iliyolenga kuwajengea uwezo
wanawake
Tunaamini kuwa mwanamke akiwezeshwa familia nzima inakuwa imewezeshwa.
Benki ya CRDB imekuwa ikimjali sana mwanamke na tumeweza kuanzisha
akaunti ya Malkia maalumu kwa ajili ya wanawake wenye malengo mbalimbali
ikiwemo ya kiujasiriamali," alieleza
Mwakilishi kutoka kampuni ya Vodacom ambao ndiyo wadhamini wakuu wa
semina na maonyesho hayo Alice Lewis alisema Vodacom inatambua mchango
wa wanawake katika maendeleo ya jamii na itaendelea kuwa mstari wa mbele
kuwasaidia kusonga mbele.
0 comments: